Kompyuta imewekwa kwa modi ya Sinzia au Lala huku ikichapisha.
Suluhisho
Usiweke kompyuta kwenye modi ya Sinzia au modi ya Lala mwenyewe wakati wa kuchapisha. Kurasa za maandishi yaliyochanganywa huenda yakachapishwa wakati ujao unapowasha kompyuta.
Unatumia kiendeshi cha kichapishi kwa kichapishi tofauti.
Suluhisho
Hakikisha kiendeshi cha kichapishi unachotumia ni cha kichapishi hiki. Angalia jina la kichapishi upande wa juu wa dirisha la kiendeshi cha kichapishi.