Kusajili Mafikio kama Kikundi kutoka Web Config

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Scan/Copy au kichupo cha Fax > Contacts

  4. Teua idadi unayotaka kusajili, na kisha ubofye Edit.

  5. Teua kikundi kutoka kwenye Type.

  6. Bofya Select kwa Contact(s) for Group.

    Mafikio yanayopatikana yameonyeshwa.

  7. Teua mafikio unayotaka kusajili kwenye kikundi, na kisha ubofye Select.

  8. Ingiza Name na Index Word.

  9. Teua iwapo umekabidhi kikundi kilichosajiliwa kwa kikundi kinachotumika mara kwa mara.

    Kumbuka:

    Mafikio yanaweza kusajiliwa kwenye vikundi anuwai.

  10. Bofya Apply.