Funga kifuniko cha waraka iwako kiko wazi.
Fungua kitengo cha kitambazaji kwa mikono miwili hadi kijifunge.
Fungua kifuniko cha tanki la wino.
Soma tahadhari za matumizi za kujaza wino kwenye skrini, na kisha uende kwenye skrini inayofuata.
Funga kifuniko kilicho kwenye tanki la wino.
Hakikisha kwamba rangi ya tangi la wino inalingana na rangi ya wino unayotaka kujaza upya.
Unaposhikilia chupa ya wino wima, geuza kifuniko polepole ili kukiondoa.
Epson inapendekeza utumie chupa halali za wino za Epson.
Chunga usimwage wino wowote.
Angalia mstari wa juu (a) kwenye tanki la wino.
Pangilia upande wa juu wa chupa ya wino kwa kituo cha kujaza, na kisha uichomeke wima kwenye kituo cha kujaza wino hadi usitishe kiotomatiki kwenye mstari wa juu.
Unapochomeka chupa ya wino kwenye kituo cha kujaza kwa rangi sahihi, wino huanza kumwagika na mtiririko husitishwa kiotomatiki wakati wino hufikia mstari wa juu.
Iwapo wino hautaanza kutiririka kwenye tanki, ondoa chupa ya wino na ujaribu kuichomeka tena. Hata hivyo, usichomeke upya chupa ya wino wakati wino umefikia mstari wa juu zaidi; vinginevyo wino unaweza kuvuja.
Unapokamilisha kujaza wino, ondoa chupa ya wino.
Usiache chupa ya wino kama imechomekwa; vinginevyo huenda chupa ikaharibika au wino unaweza kumwagika.
Iwapo wino wowote utasalia kwenye chupa ya wino, kaza kifuniko na uhifadhi cvhupa ikisimama kwa matumizi ya baadaye.
Funga kifuniko cha tanki la wino kwa usalama.
Funga kifuniko cha tanki la wino kabisa.
Funga kitengo cha kitambazaji.
Kitengo cha kitambazaji kimeundwa ili kufunga taratibu na kukataa kidogo kama kuzuia vidole vyako kukamatwa. Endelea kufunga hata ikiwa unahisi inakataa kidogo.
Fuata maagizo ya kwenye skrini ili kuweka kiwango cha wino kwa rangi ya wino uliojazwa upya.
Hata kama hutajaza wino hadi mstari wa juu wa tanki la wino, unaweza kuendelea kutumia kichapishi. Ili kufanya kichapishi chako kiendelee kufanya kazi kwa hali nzuri, hata hivyo, jaza upya tanki la wino hadi mstari wa juu na kisha uweke upya viwango vya wino mara moja.