Unaweza kuweka nenosiri la msimamizi kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Teua Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao > Mipangilio ya Usalama > Mipangilio ya Msimamizi.
Teua Nenosiri la Msimamizi > Sajili.
Ingiza nenosiri jipya.
Ingiza nenosiri tena.
Unaweza kubadilisha au kufuta nenosiri la msimamizi unapoteua Badilisha au Weka upya kwenye skrini ya Nenosiri la Msimamizi na uweke nenosiri la msimamizi.