Chapa Inatoka Kama Karatasi Tupu

Huenda nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.

Suluhisho

Tumia kipengele cha Urekebishaji wa Ubora wa Chapa. Ikiwa hujatumia kichapishi chako kwa muda mrefu, nozeli za kichwa cha kuchapishai zinaweza kuziba na huenda matone ya wino yakatoka.

Mipangilio ya uchapishaji na ukubwa wa karatasi iliyopakiwa kwenye kichapishi ni tofauti.

Suluhisho

Badilisha mipangilio ya kulingana na ukubwa wa karatasi iliyopakiwa kaenye kaseti ya karatasi. Pakia karatasi inayolingana na mipangilio ya uchapishaji kwenye kaseti ya karatasi.

Laha nyingi za karatasi zimelishwa kwenye kichapishi kwa wakati mmoja.

Suluhisho

Angalia yafuatayo ili kuzuia laha nyingi za karatasi kulishwa kwenye kichapishi kwa wakati mmoja.