Kutuma Faksi Ukitumia Kipengele cha Waraka Uliohifadhiwa

  1. Teua Kasha la Faksi kwenye skrini ya nyumbani, na kisha uteue Nyaraka Zilizohifadhiwa.

  2. Teua picha unayotaka kuchapisha kwenye skrini ya kuteua picha, na kisha uteue Anza Kutuma.

    Wakati ujumbe Futa waraka huu baada ya kutuma? umeonyeshwa, teua Ndiyo au La.

  3. Bainisha mpokeaji.

  4. Chagua kichupo cha Mipangilio ya Faksi, na kisha uweke mipangilio kama vile mbinu ya utumaji kama mipangilio inayohitajika.

  5. Donoa ili kutuma faksi.