Kusanidi Sera ya Kikundi

Sera ya kikundi kanuni moja au zaidi inayotekelezwa kwa mtumiaji au kikundi cha mtumiaji. Kichapishi hudhibiti vifurushi vya IP ambavyo vinalingana na sera zilizosanidiwa. Vifurushi vya IP vinahalalishwa kwa mpangilio wa sera ya kikundi 1 hadi 10 kisha sera chaguo-msingi.

  1. Fikia Web Config na kisha uteue kichupo cha Network Security > IPsec/IP Filtering > Basic.

  2. Bofya kichupo cha nambari unachotaka kusanidi.

  3. Ingiza thamani kwa kila kipengee.

  4. Bofya Next.

    Ujumbe wa uthibitisho unaonyeshwa.

  5. Bofya OK.

    Kichapishi kimesasishwa.