Angalia anwani ya IP ya kichapishi.
Teua ikoni ya mtandao kwenye skrini ya nyumbani ya kichapishi, na kisha uteue mbinu ya muunganisho amilifu ili kuthibitisha anwani ya IP ya kichapishi.
Pia unaweza kuangalia anwani ya IP kwa kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Zindua kivinjari Wavuti kwenye kompyuta au kifaa mahiri, na kisha uingize anwani ya IP ya kichapishi.
Umbizo:
IPv4: http://anwani ya IP ya kichapishi/
IPv6: http://[anwani ya IP ya kichapishi]/
Mifano:
IPv4: http://192.168.100.201/
IPv6: http://[2001:db8::1000:1]/
Ukitumia kifaa mahiri, unaweza pia kuendesha Web Config katika skrini ya matengenezo Epson iPrint.
Kwa vile kichapishi kinatumia cheti cha kutiwa sahihi binafsi kufikia HTTPS, onyo huonyeshwa kwenye kivinjari unapoanza Web Config; hii haionyeshi kuwa kuna tatizo na unaweza kupuuza kwa usalama.