Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.
Suluhisho
Hakikisha kwamba kiendeshi cha PC-FAX kimesakinishwa kwenye kompyuta. Kiendeshi cha PC-FAX kimesakinishwa pamoja na FAX Utility. Fuata hatua za hapa chini ili kuangalia jiwapo kimesakinishwa.
Teua Mapendeleo ya Mfumo kutoka kwenye menyu ya Apple > Vichapishi na Vitambazaji (au Chapisho na Tambazo, Kuchapisha na Faksi), na kisha uhakikishe kichapishi (faksi) kimeonyeshwa. Kichapishi (faksi) kinaonekana kama “FAX XXXX (USB)” au “FAX XXXX (IP)”. Ikiwa kichapishi (faksi) hakionekani, bofya [+] na kisha usajili printa (faksi) hiyo.
Suluhisho
Teua Mapendeleo ya Mfumo kutoka kwenye menyu ya Apple > Vichapishi na Vitambazaji (au Chapisho na Tambazo, Chapisho na Faksi), na kisha ubofye mara mbili kichapishi (faksi). Ikiwa kichapishi kimesitishwa, bofya Endelea (au Endelea Kutumia Kichapishi).
Suluhisho
Weka jina la mtumiaji na nenosiri kwenye kiendeshi cha kichapishi. Unapotuma faksi kutoka kwenye kompyuta wakati kitendaji cha usalama kinachowazuia watumiaji dhidi ya kutumia kitendaji cha faksi ya kichapishi kiwekwa, uhalalishaji wa mtumiaji unatekelezwa kwa jina la mtumiaji na nenosiri kama imewekwa kwenye kiendeshi cha kichapishi.