Kabla ya kuunda kabrasha lililoshirikiwa, angalia yafuatayo.
Kichapishi kimeunganishwa kwenye mtandao ambao kinaweza kufikia kompyuta ambapo kabrasha lililoshirikiwa litaundwa.
Kibambo cha baiti anuwai hakijajumuishwa kwenye jina la kompyuta ambapo kabrasha lililoshirikiwa litaundwa.
Wakati kibambo cha baiti anuwai kimejumuishwa kwenye jina la kompyuta, kuhifadhi faili kwenye kabrasha lililoshirikiwa kunaweza kushindikana.
Katika hali hiyo, badilisha kompyuta ambayo haijumuishi kibambo cha baiti Anuwai kwenye jina au kubadilisha jina la kompyuta.
Unapobadilisha jina la kompyuta, hakikisha umethibitisha na msimamizi mapema kwa sababu linaweza kuathiri baadhi ya mipangilio, kama vile usimamiaji wa kompyuta, ufikiaji rasilimali, nk.