> Kutatua Matatizo > Kichapishi Hakifanyi Kazi Inavyotarajiwa > Haiwezi Kuchapisha > Haiwezi Kuchapisho kutoka kwenye Windows > Ghafla, Kichapishi Hakiwezi Kuchapisha kupitia Muunganisho wa Mtandao

Ghafla, Kichapishi Hakiwezi Kuchapisha kupitia Muunganisho wa Mtandao

Huenda tatizo likawa mojawapo ya yafuatayo.

Mazingira ya mtandao yamebadilishwa.

Suluhisho

Wakati umebadilisha mazingira ya mtandao, kama vile kipanga mtandao pasiwaya au mtoa huduma, jaribu kuweka mipangilio ya mtandao ya kichapishi tena.

Unganisha kompyuta au kifaa maizi kwenye SSID moja kama kichapishi.

Tatizo fulani limetokea kwenye kifaa cha mtandao kwa muunganisho wa Wi-Fi.

Suluhisho

Zima vifaa unavyotaka kuunganisha kwenye mtandao. Subiri karibu sekunde 10, na kisha uwashe vifaa katika mpangilio ufuatao; kipanga njia pasiwaya, kompyuta au kifaa maizi, na kisha kichapishi. Sogeza kichapishi na kompyuta au kifaa mahiri karibu na kipanga njia pasiwaya ili kusaidia na mawasiliano ya mawimbi ya redio, na kisha jaribu kutengeneza mipangilio ya mtandao tena.

Kichapishi hakijaunganishwa kwenye mtandao.

Suluhisho

Teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Ukaguzi wa Muunganisho, na kisha uchapishe ripoti ya muunganisho wa mtandao. Iwapo ripoti inaonyesha kuwa muunganisho wa mtandao umeshindikana, angalia ripoti ya muunganisho wa mtandao na kisha ufuate suluhisho zilizochapishwa.

Kuna tatizo na mipangilio ya mtandao kwenye kompyuta hii.

Suluhisho

Jaribu kufikia tovuti yoyote kutoka kwenye kompyuta yako ili kuhakikisha kuwa mipangilio ya mtandao wa kompyuta yako ni sahihi. Iwapo huwezi kufikia tovuti yoyote, kuna tatizo kwenye kompyuta.

Angalia muunganisho wa mtandao wa kompyuta. Tazama hati iliyotolewa yenye kompyuta kwa maelezo.

Bado kuna shughuli inayosubiri kuchapishwa.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji. Iwapo data isiyohitajika itasalia, teua Katisha nyaraka zote kutoka kwenye menyu ya Kichapishi.

Kichapishi kinasubiri au kiko nje ya mtandao.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji.

Ikiwa kichapishi kiko nje ya mtandao au kinasubiri, futa mpangilio wa nje ya mtandao au wa kusubiri kutoka kwa menyu ya Kichapishi.

Kichapishi hakijateuliwa kuwa kichapishi chaguomsingi.

Suluhisho

Bofya mara mbili kwenye aikoni katika Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi (au Vichapishi, Vichapishi na Faksi) kisha ubofye Weka kuwa kichapishi chaguomsingi.

Kumbuka:

Ikiwa kuna aikoni nyingi za vichapishi, angalia yafuatayo ili kuchagua printa sahihi.

Mfano)

Muunganisho wa USB: Misururu ya EPSON XXXX

Muunganisho wa mtandao: Misururu ya EPSON XXXX (mtandao)

Ukisakinisha kiendesha kichapishi mara nyingi, nakala za kiendesha kichapishi huweza kuundwa. Iwapo nakala kama vile “Misururu ya EPSON XXXX (nakala 1)” zinaundwa, bofya kulia ikoni ya kiendeshi kilichonakiliwa, na kisha ubofye Ondoa Kifaa.

Lango la kichapishi halijawekwa ipasavyo.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji.

Hakikisha kwamba lango la kichapishi limewekwa ipasavyo jinsi inavyoonyeshwa hapa chini Sifa > Lango kutoka kwenye menyu ya Kichapishi.

Munganisho wa USB: USBXXX, Muunganisho wa Network: EpsonNet Print Port