Unaweza kuongeza kikundi au mtumiaji anayeruhusu ufikiaji.
Bofya kulia kwenye kabrasha na uteue Sifa.
Teua kichupo cha Usalama.
Bofya Hariri.

Bofya Ongeza hapa chini Kikundi au majina ya mtumiaji.

Ingiza kikundi au jina la mtumiaji unalotaka kuruhusu ufikiaji, na kisha ubofye Angalia Majina.
Hadhira inaongezwa kwenye jina.
Iwapo hujui jina kamili la kikundi au mtumiaji, ingiza sehemu ya jina, na kisha ubofye Angalia Majina. Majina ya kikundi au majina ya mtumiaji yanayofanana na sehemu ya jina yanaorodheshwa, na kisha unaweza kuteua jina kamili kutoka kwenye orodha.
Iwapo ni jina tu linalofafana, jina kamili likiwa limepigwa mstari linaonyeshwa kwenye Ingiza jina la kipengee ili kuteua.

Bofya Sawa.
Kwenye skrini ya Kibali, teua jina la mtumiaji linaloingizwa kwenye Kikundi au majina ya mtumiaji, teua kibali cha ufikiaji kwenye Rekebisha na kisha ubofye Sawa.

Bofya Sawa au Funga ili kufunga skrini.
Angalia iwapo faili inaweza kuandikwa au kusomwa kwenye kabrasha lililoshirikiwa kutoka kwenye kompyuta za watumiaji au vikundi vilivyo na kibali cha ufikiaji.