Kusanidi Mtandao wa IEEE 802.1X

Unapoweka IEEE 802.1X kwenye kichapishi, unaweza kuitumia kwenye mtandao uliounganishwa katika seva ya RADIUS, swichi ya LAN iliyo na kitendaji cha uhalalishaji, au eneo la ufikiaji.

  1. Fikia Web Config na kisha uteue kichupo cha Network Security > IEEE802.1X > Basic.

  2. Ingiza thamani kwa kila kipengee.

    Iwapo unataka kutumia kichapishi kwenye mtandao wa Wi-Fi, bofya Wi-Fi Setup na uteue au uingize SSID.

    Kumbuka:

    Unaweza kushiriki mipangilio kati ya Ethaneti na Wi-Fi.

  3. Bofya Next.

    Ujumbe wa uthibitisho unaonyeshwa.

  4. Bofya OK.

    Kichapishi kimesasishwa.