Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Hifadhi/Sambaza bila masharti
Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.
Fax kichupo > Save/Forward Settings > Unconditional Save/Forward
Unaweza kuweka mafikio ya kuhifadhi na kutuma mbele kwenye Kisanduku pokezi, kompyuta, kifaa cha kumbukumbu ya nje, anwani za barua pepe, makabrasha yaliyoshirikiwa, na mashine mengine ya faksi. Unaweza kutumia vipengele hivi kwa wakati mmoja. Iwapo utalemaza vipengee vyote kwenye Hifadhi/Sambaza bila masharti, kichapishi kinawekwa kuchapisha faksi zilizopokewa.
Huhifadhi faksi zilizopokewa kwenye Kisanduku pokezi cha kichapishi. Hadi hadi 100 zinaweza kuhifadhiwa. Kumbuka kuwa kuhifadhi nyaraka 100 kunaweza kuwa vigumu kulingana na masharti ya matumizi kama vile ukubwa wa faili za nyaraka zilizohifadhiwa, na kutumia vipengele mbalimbali vya kuhifadhi faksi kwa wakati mmoja.
Ingawaje faksi zilizopokewa hazichapishwi kiotomatiki, unaweza kuzitazama kwenye skrini ya kichapishi na kuchapisha tu unazohitaji. Hata hivyo, iwapo utateua Ndiyo na Uchapishe kwenye kipengee kingine, kama vile Hifadhi kwenye Kompyuta kwenye Hifadhi/Sambaza bila masharti, faksi zilizopokewa zinachapishwa kiotomatiki.
Huhifadhi faksi zilizopokewa kama faili za PDF kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi. Unaweza kuweka hii kwenye Ndiyo kwa kutumia tu FAX Utility (programu tumizi). Huwezi kuwezesha hii kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Sakinisha FAX Utility kwenye kompyuta mapema. Baada ya kuweka hii kwa Ndiyo, unaweza kubadilisha hii kuwa Ndiyo na Uchapishe kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Huhifadhi faksi zilizopokewa kama faili za PDF kwenye kifaa cha kumbukumbu ya nje kilichounganishwa kwenye kichapishi. Kuteua Ndiyo na Uchapishe huchapisha faksi zilizopokewa unapozihifadhi kwenye kifaa cha kumbukumbu.
Hati zilizopokewa uhifadhiwa kwa muda kwenye kumbukumbu ya kichapishi kabla ya nyaraka kuhifadhiwa kwenye kifaa cha kumbukumbu kilichounganishwa kwenye kichapishi. Kwa sababu hitilafu ya kumbukumbu kujaa hulemaza kutuma na kupokea faksi, weka kifaa cha kumbukumbu kikiwa kimeunganishwa kwenye kichapishi.
Hutuma mbele faksi zilizopokewa kwenye mashine mengine ya faksi, au kuzituma mbele kama faili za PDF kwenye kabrasha lililoshirikiwa kwenye mtandao au kwa anwani ya barua pepe. Faksi zilizotumwa mbele hufutwa kwenye kichapishi. Kuteua Ndiyo na Uchapishe huchapisha faksi zilizopokewa unapozituma mbele. Kwanza ongeza mafikio ya utumaji mbele kwenye orodha ya waasiliani. Ili kutuma mbele kwa anwani ya barua pepe, sanidi mipangilio ya seva ya barua pepe.
Mfikio: unaweza kuteua mafikio ya utumaji mbele kutoka kwenye orodha ya waasiliani uliyoiongeza mapema.
Ikiwa umechagua kabrasha la kushiriki kwenye mtandao au anwani ya barua pepe kama mafikio wa usambazaji, tunapendekeza kwamba ujaribu kama unaweza kutuma picha iliyochanganuliwa hadi kwa mwishilio katika hali ya uchanganuzi. Teua Changanua > Barua pepe, au Changanua > Folda/FTP ya Mtandao kutoka kwenye skrini ya nyumbani, teua mafikio, na kisha anzisha utambazaji.
Chaguo Wakati Us'zaji Um'dikana: unaweza kuteua iwapo utachapisha faksi iliyoshindikana au kuihifadhi kwenye Kisanduku pokezi.
Wakati Kisanduku pokezi kimejaa, kupokea faksi hulemazwa. Unastahili kufuta hati kwenye kisanduku pokezi punde tu zinapoangaliwa. Idadi ya nyaraka ambazo zilishindwa kusambaza imeonyeshwa kwenye
katika skrini ya nyumbani, kwa kuongezea kwenye kazi zingine zisizochakatwa.
Hutuma taarifa ya barua pepe wakati mchakato uliouteua hapa chini umekamilika. Unaweza kutumia vipengele vilivyo hapa chini kwa wakati mmoja.
Weka mafikio ya taarifa ya ukamilishaji wa mchakato.
Hutuma taarifa wakati upokeaji wa faksi umekamilika.
Hutuma taarifa wakati uchapishaji wa faksi umekamilika.
Hutuma taarifa wakati kuhifadhi faksi kwenye kifaa cha kumbukumbu kumekamilika.
Hutuma taarifa wakati usambazaji wa faksi umekamilika.