Mipangilio ya Chapa

Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Chapa

Kumbuka:
  • Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.

    Fax kichupo > Print Settings

  • Iwapo ingizo la nywila limeonyeshwa, ingiza nywila.

Upunguzaji Kiotomatiki:

Huchapisha faksi zilizopokewa kwa nyaraka za ukubwa zaidi uliopunguzwa ili kutoshea kwenye chanzo cha karatasi. Upunguzaji huenda usiwezekane kulingana na data iliyopokewa. Ikiwa kipengele hiki kimezimwa, hati kubwa huchapishwa kwa ukubwa wake asili kwenye karatasi nyingi, au ukurasa tupu wa pili unaweza kutolewa.

Mipangilio ya Kugawanya Kurasa:

Huchapisha faksi zilizopokewa kwa ya kugawa ukurasa wakati ukubwa wa nyaraka ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi iliyopakiwa kwenye kichapishi.

Uzungushaji Kiotomatiki:

Huzungusha faksi zilizopokewa kama mwelekeo wa ulalo nyaraka za ukubwa wa A5 ili iweze kuchapishwa kwenye karatasi ya ukubwa wa A5. Mpangilio huu unatekelezwa wakati mpangilio wa ukubwa wa karatasi kwa angalau chanzo kimoja cha karatasi kinachotumika kwa kuchapisha faksi kimewekwa kwa A5.

Kwa kuteua Zima, faksi zilizopokewa kama nyaraka za ukubwa wa mwelekeo wa ulalo A4, zinachukuliwa kuwa faksi za ukubwa wa A4 na kuchapishwa vivyo hivyo.

Angalia mipangilio ya chanzo cha karatasi kwa kuchapisha faksi na ukubwa wa karatasi kwa vyanzo vya karatasi kwenye menyu zifuatazo katika Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Mipangilio Chanzo Karatasi.

  • Mipangilio ya Uchaguaji Oto

  • Mipangilio ya Karatasi > Ukubwa wa Karatasi

Ongeza Maelezo ya Mapokezi:

Maelezo ya mapokezi ya uchapisho kwenye faksi iliyopokewa, hata iwapo mtumaji hajaweka maelezo ya kichwa. Maelezo ya mapokezi yanajumuisha tarehe na saa, Kitambulisho cha mtumaji, Kitambulisho cha mapokezi (kama vile “#001”) na nambari ya ukurasa (kama vile “P1”). Kwa kujumuisha Kitambulisho cha mapokezo yaliyochapishwa kwenye faksi iliyopokelewa, unaweza kuangalia kumbukumbu ya wasilisho kwenye ripoti ya faksi na historia ya kazi ya faksi. Wakati Mipangilio ya Kugawanya Kurasa imewezeshwa, nambari ya kugawanya ukurasa pia inajumuishwa.

Pande 2:

Huchapisha kurasa anuwai za faksi zilizopokewa katika pande zote za karatasi.

Muda wa Uchapishaji Kuanza:

Teua chaguao ili kuanza kuchapisha faksi za kupokea.

  • Kurasa Zote Zimepokewa: Uchapishaji huanza baada ya kupokea kurasa zote. Ili kuanza kuchapisha kutoka kwenye ukurasa wa kwanza au ukurasa wa mwisho hutegemea na mpangilio wa kipengele cha Kitita cha Ulinganisho. Tazama ufafanuzi wa Kitita cha Ulinganisho.

  • Ukurasa wa Kwanza Umepokewa: Huanza kuchapisha ukurasa wa kwanza kupokewa, na kisha huchapisha kwa utaratibu kama kurasa zinapokewa. Iwapo kichapishi hakiwezi kuchapisha, kama vile wakati inachapisha kazi nyingine, kichapishi huanza kuchapisha kurasa zilizopokewa kama bechi zinapopatikana.

Kitita cha Ulinganisho:

Kwa kuwa ukurasa wa kwanza unachapishwa mwisho (towe upande wa juu), nyaraka zilizochapishwa zinawekwa pamoja kwenye utaratibu sahihi wa ukurasa. Wakati kumbukumbu ya printa inapungua, kipegele hiki huenda kizipatikane.

Saa ya Kusitisha Chapa:
Saa ya Kusitisha Chapa

Wakati wa kipindi kilichobainishwa cha muda, kichapishi huhifadhi nyaraka zilizopokewa kwenye kumbukumbu ya kichapishi bila kuzichapisha. Kipengele hiki kinaweza kutumiwa kuzuia kelele usiku au kuzuia hati za usiri kufichuliwa wakati uko mbali. Kabla ya kutumia kipengele hiki, hakikisha kuna kumbukumbu ya kutosha. Hata kabla ya wakati wa kuanzisha upya, unaweza kuangalia na kuchapisha hati zilizopokewa kutoka Hali ya Kazi kwenye skrini ya nyumbani.

Muda wa Kukomesha

Husitisha kuchapisha nyaraka.

Wakati wa Kuanzisha upya

Huwasha upya uchapishaji nyaraka kiotomatiki.

Hali Tulivu:

Hupunguza kelele ambazo kichapishi hutoa unapochapisha faksi, hata hivyo, kasi ya kuchapisha inaweza kupunguzwa.