Mipangilio ya Kawaida:

Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Mipangilio ya Kawaida

Kumbuka:

Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.

  • Kichupo cha Fax > Fax Box > Inbox

  • Kichupo cha Fax > Save/Forward Settings > Common Settings

Mipangilio ya Kikasha pokezi:
Chaguo wakati kumbukumbu imejaa:

Unaweza kuteua operesheni ya kuchapisha faksi iliyopokewa au kukataa kuipokea wakati kumbukumbu ya Kisanduku pokezi imejaa.

Mipangilio ya Nenosiri la Kisanduku pokezi:

Nenosiri hulinda Kisanduku pokezi ili kuwazuia watumiaji dhidi ya kutazama faksi zilizopokewa. Teua Badilisha ili kubadilisha nenosiri, na uchague Weka upya ili kughairi ulinzi wa nenosiri. Wakati unabadilisha au kuweka upya nenosiri, unahitaji nenosiri la sasa.

Huwezi kuweka nenosiri wakati Chaguo wakati kumbukumbu imejaa imewekwa kwa Pokea na uchapishe faksi.

Tuma Mada ya Kusambaza:

Unaweza kubainisha mada kwa barua pepe unapotuma mbele barua pepe kwenye anwani ya barua pepe.