Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Matengenezo
Matengenezo
Urekebishaji wa Ubora wa Chapa
Teua kipengele hiki iwapo kuna matatizo yoyote kwa machapisho yako. Unaweza kuangalia nozeli zilizoziba na usafishe kichwa cha kichapishi ikihitajika, na kisha urekebishe baadhi ya parameta ili kuimarisha ubora.
Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa
Teua kipengele hiki ili iangalie kama nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.Kichapishi huchapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli.
Usafishaji Kichwa cha Chapa
Teua kipengele hiki ili kusafisha nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha.
Usafishaji wa Nishati
Teua kipengele hiki ili kubadilisha wino wote ulio ndani ya tyubu ya wino. Wino zaidi unatumika kuliko wakati wa usafishaji wa kawaida. Tazama “Maelezo Husiani” hapa chini kwa maelezo zaidi kuhusu ksutumia kipengele hiki.
Upangiliaji wa Kichwa cha Kuchapisha
Teua kipengele hiki ili kurekebisha kichwa cha kuchapisha ili kuimarisha ubora wa uchapishaji.
Mpangilio uliopigwa Mstari
Teua kipengele hiki ili kupanga mistari ya wima.
Upangiliaji Kimlalo
Teua kipengele hiki iwapo bendi ya mlalo itaonekana kwa vipindi vya kila mara kwenye machapisho yako.
Jaza Wino
Teua kipengele hiki ili uweke upya viwango vya wino kwa 100% unapojaza tangi la wino upya.
Uwekaji wa Kiwango cha Wino
Teua kipengele hiki ili uweke kiwango cha wino kulingana na wino halisi unaosalia.
Usafishaji wa Mwongozo wa Karatasi
Teua kipengele hiki iwapo kuna madoa ya wino kwenye rola za ndani.Kichapishi huingiza karatasi ili kusafisha rola za ndani.
Ondoa Karatasi
Tumia kipengele hiki ikiwa bado kuna vipande vilivyoraruka vya karatasi ndani ya kichapishi hata baada ya kuondoa karatasi iliyokwama.Kichapishi huongeza nafasi zaidi kati ya kichwa cha kuchapisha na sehemu ya karatasi ili kurahisisha kuondoa vipande vya karatasi vilivyoraruka.
Usafishaji wa Mara kwa Mara
Kichapishi hutekeleza kiotomatiki Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa na Usafishaji Kichwa cha Chapa kulingana na kipindi maalum cha muda. Teua On ili kudumisha ubora unaostahili wa chapisho. Chini ya hali kama hizi, tekeleza Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa na Usafishaji Kichwa cha Chapa mwenyewe.
Matatizo ya uchapishaji
Wakati Zima imeteuliwa kwa Usafishaji wa Mara kwa Mara
Unapochapisha kwa ubora wa juu, kama vile picha
Wakati ujumbe wa Usafishaji Kichwa cha Chapa umeonyeshwa kwenye skrini ya LCD