Kupata Cheti Kilichotiwa sahihi cha CA

Ili kupata cheti kilichotiwa sahihi cha CA, unda CSR (Ombi la Kutia sahihi kwenye Cheti) na uitekeleze kwa mamlaka ya cheti. Unaweza kuunda CSR kutumia Web Config na kompyuta.

Fuata hatua ili kuunda CSR na upate cheti kilichotiwa sahihi cha Web Config. Unapounda CSR ukitumia Web Config, chetikipo kwenye umbizo la PEM/DER.

  1. Fikia Web Config, na kisha uteue kichupo cha Network Security. Pili, teua SSL/TLS > Certificate au IPsec/IP Filtering > Client Certificate au IEEE802.1X > Client Certificate.

    Chochote unachochagua, unaweza kupata cheti sawa na kukitumia kwa kawaida.

  2. Bofya Generate ya CSR.

    Uundaji ukurasa wa CSR umefunguliwa.

  3. Ingiza thamani kwa kila kipengee.

    Kumbuka:

    Urefu wa ufnguo na ufupisho unaopatikana hutofautiana kwa cheti cha mamlaka. Unda ombi kulingana na kanuni za mamlaka ya kila cheti.

  4. Bofya OK.

    Ujumbe wa ukamilisho umeonyeshwa.

  5. Chagua kichupio cha Network Security. Pili, teua SSL/TLS > Certificate, au IPsec/IP Filtering > Client Certificate au IEEE802.1X > Client Certificate.

  6. Bofya mojawapo ya vitufe vilivyopakuliwa vya CSR kulingana na umbizo lililobainishwa kwa kila mamlaka ya cheti ili kupakua CSR kwenye kompyuta.

    Muhimu:

    Usizalishe tena CSR. Ukifanya hivyo, huenda usiweze kuleta CA-signed Certificate kilichotolewa.

  7. Tuma CSR kwenye mamlaka ya cheti na upate CA-signed Certificate.

    Fuata kanuni za kila mamlaka ya cheti kwenye mbinu na fomu ya utumaji.

  8. Hifadhi CA-signed Certificate kilichotolewa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi.

    Kupata CA-signed Certificate kunakamilika unapohifadhi cheti katika mafikio.