> Kutatua Matatizo > Ni Wakati wa Kujaza tena Wino > Kujaza Matangi ya Wino Upya

Kujaza Matangi ya Wino Upya

  1. Fungua kitengo cha kitambazaji wakati jalada la waraka limefungwa.

  2. Fungua kifuniko cha tanki la wino.

    Soma tahadhari zote za matumizi kwa kujaza wino kwenye skrini ya LCD, na kidha udonoe Endelea.

  3. Fungua kifuniko cha tanki la wino.

    Muhimu:

    Hakikisha kwamba rangi ya tangi la wino inalingana na rangi ya wino unayotaka kujaza upya.

  4. Unaposhikilia chupa ya wino wima, geuza kifuniko polepole ili kukiondoa.

    Muhimu:
    • Epson inapendekeza utumie chupa halali za wino za Epson.

    • Chunga usimwage wino wowote.

  5. Angalia mstari wa juu (a) kwenye tanki la wino.

  6. Pangilia upande wa juu wa chupa ya wino kwa kituo cha kujaza, na kisha uichomeke wima kwenye kituo cha kujaza wino kwenye mstari wa juu.

    Unapochomeka chupa ya wino kwenye kituo cha kujaza kwa rangi sahihi, wino huanza kumwagika na mtiririko husitishwa kiotomatiki wakati wino hufikia mstari wa juu.

    Iwapo wino hautaanza kutiririka kwenye tanki, ondoa chupa ya wino na ujaribu kuichomeka tena. Hata hivyo, usichomeke upya chupa ya wino wakati wino umefika mstari wa juu; vinginevyo wino unaweza kuvuja.

    Muhimu:

    Usiruhusu sehermu ya juu ya chupa ya wino kugonga vifaa vyovyote baada ya kuondoa kifuniko; vinginevyo wino unaweza kumwagika.

  7. Unapokamilisha kujaza wino, ondoa chupa ya wino.

    Muhimu:

    Usiache chupa ya wino kama imechomekwa; vinginevyo huenda chupa ikaharibika au wino unaweza kumwagika.

    Kumbuka:

    Iwapo wino wowote utasalia kwenye chupa ya wino, kaza kifuniko na uhifadhi cvhupa ikisimama kwa matumizi ya baadaye.

  8. Funga kifuniko cha tanki la wino kwa usalama.

  9. Funga kifuniko cha tanki la wino kabisa.

  10. Funga kitengo cha kitambazaji.

    Kwa usalama, kitengo cha kitambazaji kinafungwa kwa hatua nne.

    Kumbuka:

    Kitengo cha kitambazaji hakiwezi kufunguliwa kutoka katika nafasi iliyoonyeshwa hapa chini. Kifunge kabisa kabla ya kukifungua.

  11. Fuata maagizo ya kwenye skrini ili kuweka kiwango cha wino kwa rangi ya wino uliojawa upya.

    Muhimu:

    Hata kama hutajaza wino hadi mstari wa juu wa tanki la wino, unaweza kuendelea kutumia kichapishi. Ili kufanya kichapishi chako kiendelee kufanya kazi kwa hali nzuri, hata hivyo, jaza upya tanki la wino hadi mstari wa juu na kisha uweke upya viwango vya wino mara moja.