Kuunda Mipangilio ya Kutuma na Kupokea Faksi kwenye Kompyuta

Ili kutuma na kupokea faksi kwenye kompyuta, FAX Utility inafaa kusakinishwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwa mtandao au kebo ya USB.

Kufanya Mpangilio wa Hifadhi kwenye Kompyuta Kupokea Faksi

Unaweza kupokea faksi kwenye kompyuta kwa kutumia FAX Utility. Sakinisha FAX Utility kwenye kompyuta na kuunda mpangilio. Kwa maelezo, tazama Basic Operations kwenye msaada wa FAX Utility (yanayoonyeshwa kwenye dirisha kuu).

Kipengee kilicho hapa chini cha mpangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi kimewekwa kwa Ndiyo, na faksi zilizopokewa zinaweza kuhifadhiwa kwenye kompyuta.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Faksi Towe > Hifadhi kwenye Kompyuta

Kufanya Mpangilio wa Hifadhi kwenye Kompyuta Pia Kuchapisha ili Kupokea Faksi

Unaweza kuunda mpangilio kuchapisha faksi zilizopokewa kwenye kichapishi na pia kuzihifadhi kwenye kompyuta.

  1. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani kwenye paneli dhibiti.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.

  3. Teua Faksi Towe > Hifadhi kwenye Kompyuta > Ndiyo na Uchapishe.

Kufanya Mpangilo wa Hifadhi kwenye Kompyuta Kutopokea Faksi

Ili kuweka kichapishi kutohifadhi faksi zilizopokewa kwenye kompyuta, badilisha mipangilio kwenye kichapishi.

Kumbuka:

Pia unaweza kubadilisha mipangilio kwa kutumia FAX Utility. Hata hivyo, iwapo kuna faksi zozote ambazo hazijahifadhiwa kwenye kompyuta, kipengele hakifanyi kazi.

  1. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani kwenye paneli dhibiti.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.

  3. Teua Faksi Towe > Hifadhi kwenye Kompyuta > La.