Kuchapisha Taswira fifi

Unaweza kuchapisha taswira fifi kama vile “Ya siri” au ruwaza ya kutonakili kwenye machapisho yako. Iwapo utachapisha kwa ruwaza ya kutonakili, herufi zilizofichwa huonekana zinaponakiliwa ili kutofautisha nakala asili kutoka kwenye nakala.

Ruwaza ya Kizuia Nakala inapatikana chini ya masharti yafuatayo:

  • Aina ya Karatasi: Karatasi tupu, karatasi ya nakala, Karatasi ya kichwa cha barua

  • Bila kingo: Haijateuliwa

  • Ubora: Wastani

  • Uchapishaji wa Pande 2: Zima, Mwongozo (Kujalidi ukingo mrefu), au Mwongozo (Kujalidia ukingo mfupi)

  • Usahihishaji wa Rangi: Otomatiki

Kumbuka:

Unaweza pia kuongeza taswira fifi yako mwenyewe ya ruwaza ya kutonakili.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Trei ya Karatasi

  2. Fungua faili unayotaka kuchapisha.

  3. Chagua Chapisha au Usanidi wa Uchapishaji katika menyu ya Faili.

  4. Teua kichapishi chako.

  5. Teua Mapendeleo au Sifa ili uende kwa dirisha la kiendeshi cha printa.

  6. Bofya Vipengele vya Taswira fifi kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi na uteue ainaya ruwaza ya aina isiyo ya nakala au taswira fifi unayotaka kutumia.

  7. Bofya Mipangilio ili kubadilisha maelezo kama vile ukubwa, uzito, au nafasi ya ruwaza au alama.

  8. Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.

    Kichupo cha Kuu

    Kichupo cha Chaguo Zaidi

  9. Bofya Chapisha.