Unaweza kutumia mbinu zozote kati ya zifuatazo kutambaza ukitumia kichapishi hiki.
Unaweza kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kompyuta.
Unaweza kutuma taswira zilizotambazwa kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hadi huduma ya wingu ambayo imesajiliwa mapema.
Unaweza kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi, kwa kutumia kipengele cha WSD.
Unaweza kuhifadhi taswira zilizotambazwa moja kwa moja kwenye kifaa maizi kama vile simu mahiri au kompyuta kibao kwa kutumia programu ya Epson iPrint kwenye kifaa maizi.