Teua kipengele hiki ili iangalie kama nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.Kichapishi huchapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli.
Teua kipengele hiki ili kusafisha nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha.
Teua kipengele hiki ili kubadilisha wino wote ulio ndani ya tyubu za wino. Wino zaidi unatumika kuliko wakati wa usafishaji wa kawaida. Tazama “Maelezo Husiani” hapa chini kwa maelezo zaidi kuhusu ksutumia kipengele hiki.
Teua kipengele hiki ili kurekebisha kichwa cha kuchapisha ili kuimarisha ubora wa uchapishaji.
Ulainishaji Wima
Teua kipengele hiki iwapo machapisho yako yataonekana yakiwa na ukungu au maandishi na mistari hailingani.
Upangiliaji Kimlalo
Teua kipengele hiki iwapo bendi ya mlalo itaonekana kwa vipindi vya kila mara kwenye machapisho yako.
Teua kipengele hiki ili uweke kiwango cha wino kulingana na wino halisi unaosalia.