Kuangalia Hali Ya Muunganisho

Tumia EPSON Status Monitor kuangalia hali ya muunganisho ya kompyuta na kichapishi.

  1. Teua Mapendeleo ya Mfumo kwenye menyu ya Apple > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi), na kisha uteue kichapishi.

  2. Bofya Chaguo na Vifaa > Huduma > Fungua Huduma ya Printa.

  3. Bofya EPSON Status Monitor.

Viwango vya wino unaosalia vikionyeshwa, muunganisho umefaulu kuwekwa kati ya kompyuta na kichapishi.

Angalia yafuatayo ikiwa muunganisho haujawekwa.