Kuunda Mipangilio ya Kutuma na Kupokea Faksi kwenye Kompyuta

Ili kutuma na kupokea faksi kwenye kompyuta, FAX Utility inafaa kusakinishwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwa mtandao au kebo ya USB.

Kuunda Mpangilio wa Hif'hi k. Kompyuta Kupokea Faksi

Unaweza kupokea faksi kwenye kompyuta kwa kutumia FAX Utility. Sakinisha FAX Utility kwenye kompyuta teja na uunde mpangilio. Kwa maelezo, tazama Basic Operations kwenye msaada wa FAX Utility (yanayoonyeshwa kwenye dirisha kuu).

Kipengee cha mpangilio kilicho hapa chini kwenye paneli dhibiti ya kichapishi kimewekwa kwa Ndiyo, na faksi zilizopokewa zinaweza kuhifadhiwa kwenye kompyuta.

Mipangilio > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Hif'hi k. Kompyuta

Kufanya Mpangilio wa Hif'hi k. Kompyuta ili Pia Kuchapisha kwenye Kichapishi ili Kupokea Faksi

Unaweza kuunda mpangilio ili kuchapisha faksi zilizopokewa kwenye kichapishi na pia kuzihifadhi kwenye kompyuta.

  1. Chagua Mipangilio kwenye skrini ya mwanzo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Chagua Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.

  3. Chagua Hif'hi k. Kompyuta > Ndiyo na Uchapishe.

Kuunda Mpangilio wa Hif'hi k. Kompyuta Kutopokea Faksi

Ili kuweka kichapishi kutopokea faksi kwenye kompyuta, badilisha mipangilio kwenye kichapishi.

Kumbuka:

Pia unaweza kubadilisha mipangilio kwa kutumia FAX Utility. Hata hivyo, iwapo kuna faksi zozote ambazo hazijahifadhiwa kwenye kompyuta, kipengele hakifanyi kazi.

  1. Chagua Mipangilio kwenye skrini ya mwanzo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Chagua Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.

  3. Teua Hif'hi k. Kompyuta > La.