> Kuchapisha > Kuchapisha Nyaraka > Kuchapisha kutoka kwenye Kompyuta — Windows > Kuchapisha ili Itoshee Katika Ukubwa wa Karatasi

Kuchapisha ili Itoshee Katika Ukubwa wa Karatasi

Teua ukubwa wa karatasi uliyopakia kwenye kichapishi kama mpangilio wa Ukubwa wa Karatasi Elekea.

Kumbuka:

Kipengele hiki hakipatikani na uchapishaji usio na mipaka.

  1. Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi cha Chaguo Zaidi, chukua hatua zifuatazo.

    • Ukubwa wa Waraka: teua ukubwa wa karatasi uliyoweka kwenye mipangilio ya programu.
    • Karatasi ya Zao: teua ukubwa wa karatasi uliyoipakia katika kichapishi.
      Tosheleza kwenye Ukurasa huteuliwa kiotomatiki.
    Kumbuka:

    Bofya Katikati ili kuchapisha tasiwra iliyopunguzwa katikati ya karatasi.

  2. Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.

  3. Bofya Chapisha.