Web Config ni programu ambayo huendeshwa katika kivinjari cha wavuti, kama vile Microsoft Edge na Safari, kwenye kompyuta na kifaa mahiri. Unaweza kuthibitisha hali ya printa au kubadilisha huduma ya ntandao na mipangilio ya printa. Ili utumie Web Config, unganisha printa na kompyuta au kifaa kwenye mtandao mmoja.
Vivinjari vifuatavyo vinakubaliwa. Tumia toleo jipya.
Microsoft Edge, Internet Explorer, Firefox, Chrome, Safari
Huenda ukaombwa kuingiza nenosiri la msimamizi unapoendesha Web Config. Tazama maelezo husika hapa chini kupata maelezo zaidi.