Kuendesha Web Config Kwenye Kivinjari Wavuti

  1. Angalia anwani ya IP ya kichapishi.

    Shikilia chini kitufe cha kwa angalau sekunde 5 ili uchapishe karatasi ya hali ya mtandao, na kisha uangalie anwani ya IP ya kichapishi.

  2. Zindua kivinjari Wavuti kwenye kompyuta au kifaa mahiri, na kisha uingize anwani ya IP ya kichapishi.

    Umbizo:

    IPv4: http://anwani ya IP ya kichapishi/

    IPv6: http://[anwani ya IP ya kichapishi]/

    Mifano:

    IPv4: http://192.168.100.201/

    IPv6: http://[2001:db8::1000:1]/

    Kumbuka:

    Ukitumia kifaa mahiri, unaweza pia kuendesha Web Config kutoka katika skrini ya maelezo ya bidhaa ya Epson Smart Panel.

    Kwa vile kichapishi kinatumia cheti cha kutiwa sahihi binafsi kufikia HTTPS, onyo huonyeshwa kwenye kivinjari unapoanza Web Config; hii haionyeshi kuwa kuna tatizo na unaweza kupuuza kwa usalama.