> Kutatua Matatizo > Programu au Kiendeshi cha Printa Hakifanyi Kazi Vizuri > Hakiwezi Kuchapisha Ingawa Muunganisho Umewekwa (Windows)

Hakiwezi Kuchapisha Ingawa Muunganisho Umewekwa (Windows)

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson hakijasakinishwa.

Suluhisho

Iwapo kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson cha (EPSON XXXXX) hakijasakinishwa, utendaji unaopatikana una kipimo. Tunapendekeza kutumia kiendeshi cha kichapishi cha Epson halali.

Kuna tatizo na programu au data.

Suluhisho

  • Ikiwa unachapisha picha yenye data kubwa, huenda komyuta ikakosa nafasi ya kutosha kwenye kumbukumbu. Chapisha picha kwa msongo wa chini au ukubwa mdogo.

  • Ikiwa umejaribu suluhu zote na hujafakiniwa kutatua tatizo, jaribu kuondoa kisha kusakinisha tena kiendesha kichapishi

Kuna tatizo na hali ya kichapishi.

Suluhisho

Bofya EPSON Status Monitor 3 kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi Utunzaji, na kisha uangalie hali ya kichapishi. Ikiwa EPSON Status Monitor 3 imelemazwa, bofya Mipangilio Iliyorefushwa kwenye kichupo cha Utunzaji, na kisha uteue Wezesha EPSON Status Monitor 3.

Bado kuna shughuli inayosubiri kuchapishwa.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji. Iwapo data isiyohitajika itasalia, teua Katisha nyaraka zote kutoka kwenye menyu ya Kichapishi.

Kichapishi kinasubiri au kiko nje ya mtandao.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji.

Ikiwa kichapishi kiko nje ya mtandao au kinasubiri, futa mpangilio wa nje ya mtandao au wa kusubiri kutoka kwa menyu ya Kichapishi.

Kichapishi hakijateuliwa kuwa kichapishi chaguomsingi.

Suluhisho

Bofya mara mbili kwenye aikoni katika Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi (au Vichapishi, Vichapishi na Faksi) kisha ubofye Weka kuwa kichapishi chaguomsingi.

Kumbuka:

Ikiwa kuna aikoni nyingi za vichapishi, angalia yafuatayo ili kuchagua printa sahihi.

Mfano)

Muunganisho wa USB: Misururu ya EPSON XXXX

Muunganisho wa mtandao: Misururu ya EPSON XXXX (mtandao)

Ukisakinisha kiendesha kichapishi mara nyingi, nakala za kiendesha kichapishi huweza kuundwa. Iwapo nakala kama vile “Misururu ya EPSON XXXX (nakala 1)” zinaundwa, bofya kulia ikoni ya kiendeshi kilichonakiliwa, na kisha ubofye Ondoa Kifaa.

Lango la kichapishi halijawekwa ipasavyo.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji.

Hakikisha kwamba lango la kichapishi limewekwa ipasavyo jinsi inavyoonyeshwa hapa chini Sifa > Lango kutoka kwenye menyu ya Kichapishi.

Munganisho wa USB: USBXXX, Muunganisho wa Network: EpsonNet Print Port