Wakati unahitaji kuhifadhi kichapishi au kukihamisha au kwa ukarabati, fuata hatua zilizo hapa chini za kupakia kichapishi.
Pia unaweza kutazama taratibu katika M'ozo Video Mt'ni. Fikia tovuti inayofuata.
Zima kichapishi kwa kubonyeza kitufe cha
.
Hakikisha taa ya nishati imezima, na kisha uchomoe waya ya nishati.
Chomoa waya ya nishati wakati taa ya nishati imezimwa. La sivyo, kichwa cha kuchapisha hakitarudi kwenye mkao wake na wino utakauka, na huenda isiweze kuchapisha.
Tenganisha kebo zote kama vile waya ya nishati na kebo ya USB.
Ondoa karatasi zote kutoka kwa kichapishi.
Fungua kifuniko cha kichapishi.
Weka kufuli la usafirishaji kwa mkao wa kufungwa (Usafirishaji).
Kufuli la usafirishaji husitisha usambazaji wa wino ili kuzuia umwagikaji wa wino unaposafirisha au kuhifadhi.
Iwapo kichwa cha kuchapisha hakipo katika mkao ulioonyeshwa hapa chini, kisogeze kwa mkono.

Funga kichwa cha kuchapisha kwenye kesi ukitumia utepe.

Hakikisha umesakinisha kifuniko kilicho kwenye tangi la wino vizuri.

Funga kifuniko cha tanki la wino kwa usalama.

Funga kifuniko cha kichapishi.

Andaa kupakua kichapishi kama inavyoonyeshwa hapa chini.

Weka kichapishi kwenye mkoba wa plastiki uliosambazwa kwa ajili ya kusafirisha na uufunge.
Fuga printa kwenye sanduku lake kwa kutumia vifaa vya kukinga.

Wakati unabeba kichapishi, kiinue katika mkao thabiti. Kuinua kichapishi katika mkao usio thabiti kunaweza kusababisha majeraha.
Unapoinua printa, weka mikono yako katika maeneo yaliyoonyeshwa hapa chini. Usishike kichapishi kwenye sehemu ya mbele au nyuma.

Wakati wa kuhifadhi au kusafirisha chupa ya wino, usiinamishe chupa na usiigongeshe au kuiweka mahali penye mabadiliko ya hali joto.La sivyo, wino unaweza kuvuja hata kama kifuniko kilicho kwenye chupa ya wino kimekazwa vizuri.Hakikisha umeweka chupa ya wino ikiwa imesimama wakati unakaza kifuniko, na utahadhari ili uzuie wino usivuje wakati unasafirisha chupa, kwa mfano, kuweka chupa kwenye mkoba.

Usiweke chupa za wino zilizofunguliwa ndani ya sanduku pamoja na printa.

Wakati mwingine utatumia kichapishi, hakikisha umeondoa utepe wa unaokinga kichwa cha kuchapisha na uweke kufuli la usafirishaji katika mkao wa kufunguliwa (Chapisha). Ikiwa ubora wa uchapishaji utapungua wakati ujao utakaochapisha, safisha na ulinganishe kichwa cha kuchapisha.