Hakikisha kuwa umesajili ukubwa na aina ya karatasi kwenye skrini inayoonyeshwa unapopakia karatasi. Printa hukujulisha wakati maelezo yaliyosajiliwa na mipangilio ya kuchapisha inatofautiana. Hii hukuzuia kupoteza karatasi na wino kwa kuhakikisha kwamba huchapishi kwenye ukubwa usiofaa wa karatasi au kuchapisha kwa ubora mbaya wa chapisho kutoka na kutumia mipangilio ambayo hailingani na aina ya katarasi.

Iwapo ukubwa wa karatasi unaoonyeshwa ni tofauti na karatasi iliyopakiwa, teua Badilisha ili kufanya mabadiliko. Teua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi, angalia mipangilio, na kisha ubonyeze kitufe cha OK. Iwapo mipangilio inalingana na karatasi iliyopakiwa, teua Thibitisha.
Iwapo hutaki kuonyesha skrini ya mipangilio ya ukurasa kiotomatiki unapopakia karatasi, teua menyu kwenye skrini ya mwanzo kama ilivyoelezwa hapa chini.
Mipangilio > Usanidi wa Printa > Mip'o Chanzo Karatasi > Ony. Ot. Usan'i/ Kar. > Zima.