Kuongeza Kitambazaji cha Mtandao

Ili kutumia kitambazaji cha mtandao, ongeza kitambazaji kwa kutumia kiendesha kitambazaji “Epson Scan 2”.

  1. Anzisha Epson Scan 2.

    • Windows 10/Windows Server 2016
      Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue EPSON > Epson Scan 2.
    • Windows 8.1/Windows 8/Windows Server 2012 R2/Windows Server 2012
      Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.
    • Windows 7/Windows Vista/Windows XP/Windows Server 2008 R2/Windows Server 2008/Windows Server 2003 R2/Windows Server 2003
      Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote au Programu > EPSON > Epson Scan 2.
    • Mac OS
      Teua Nenda > Programu > Epson Software > Epson Scan 2.
  2. Kwenye skrini ya Mipangilio ya Kichanganuzi, bofya Ongeza.

    Kumbuka:
    • Iwapo Ongeza imefifishwa, bofya Wezesha Hariri.

    • Iwapo skrini kuu ya Epson Scan 2 imeonyeshwa, tayari imeunganishwa kwenye kitambazaji. Iwapo unataka kuunganisha kwenye mtandao mwingine, teua Kichanganuzi > Mipangilio ili kufungua skrini ya Mipangilio ya Kichanganuzi.

  3. Ongeza kitambazaji cha mtandao. Ingiza vipengee vifuatavyo, na kisha ubofye Ongeza.

    • Modeli: Teua kitambazaji unachotaka kuunganishia.
    • Jina: Weka jina la kitambazaji. Unaweza kuingiza hadi vibambo 32.
    • Tafuta Mtandao: Wakati kompyuta na kitambazaji vipo kwenye mtandao sawa, anwani ya IP huonyeshwa. Iwapo haijaonyeshwa, bofya kitufe cha . Iwapo bado anwani ya IP haijaonyeshwa, bofya Weka anwani, na kisha uingize anwani ya IP moja kwa moja.
  4. Teua kitambazaji kwenye skrini ya Mipangilio ya Kichanganuzi, kisha ubofye Sawa.