Unaweza kuchapisha hati, barua pepe, picha au kurasa za wavuti pasiwaya moja kwa moja kutoka katika simu au kompyuta yako kibao Android (Android v4.4 au jipya zaidi). Kwa kudonoa mara chache tu, kifaa chako cha Android kinaweza kugundua kichapishi cha Epson ambacho kimeunganishwa kwenye mtandao sawa.
Uendeshaji unaweza kutofautiana kulingana na kifaa.
Pakia karatasi katika kichapishi.
Kwenye kifaa chako cha Android, sakinisha kiendelezi cha Epson Print Enabler kutoka Google Play.
Unganisha kifaa chako cha Android kupitia kipanga njia pasiwaya.
Nenda katika Mipangilio kwenye kifaa cha Android, teua Kuchapisha kisha wezesha Epson Print Enabler.
Kutoka katika programu ya Android kama vile Chrome, donoa aikoni ya menyu na uchapishe kilicho kwenye skrini.
Iwapo hutaona kichapishi chako, donoa Vichapishi Vyote na uteue kichapishi chako.