Matengenezo

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Mipangilio > Matengenezo

Ukaguaji Nozeli:

Teua kipengele hiki ili iangalie kama nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.Kichapishi huchapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli.

Usafishaji Kichwa:

Teua kipengele hiki ili kusafisha nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha.

Usafishaji wa Nishati:

Teua kipengele hiki cha usafishaji wa nishati ili kusafisha nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha. Wino zaidi unatumika kuliko wakati wa usafishaji wa kawaida. Tazama “Maelezo Husiani” hapa chini kwa maelezo zaidi kuhusu ksutumia kipengele hiki.

Ulainishaji Kichwa:

Teua kipengele hiki ili kurekebisha kichwa cha kuchapisha ili kuimarisha ubora wa uchapishaji.

  • Upangiliaji Wima

    Teua kipengele hiki iwapo machapisho yako yataonekana yakiwa na ukungu au maandishi na mistari hailingani.

  • Upangiliaji Kimlalo

    Teua kipengele hiki iwapo bendi ya mlalo itaonekana kwa vipindi vya kila mara kwenye machapisho yako.

Jaza Wino:

Teua kipengele hiki ili uweke upya viwango vya wino kwa 100% unapojaza tanki la wino.

Weka Kiwango cha wino:

Teua kipengele hiki ili uweke kiwango cha wino kulingana na wino halisi unaosalia.

Usfshaji Mwongzo wa Krtasi:

Teua kipengele hiki iwapo kuna madoa ya wino kwenye rola za ndani.Kichapishi huingiza karatasi ili kusafisha rola za ndani.