Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Kuingiza SSID na Nenosiri

Unaweza kusanidi kikuli mtanfdao wa Wi-Fi kwa kuingiza maelezo muhimu ya kuunganisha kwenye kipanga njia pasiwaya kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Ili kusanidi kwa kutumia mbinu hii, unahitaji SSID na nenosiri kwa kipanga njia pasiwaya.

Kumbuka:

Iwapo unatumia eneo la kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio yake chaguo-msingi, SSID na nywila ziko kwenye lebo. Iwapo hufahamu SSID na nywila, tazama nyaraka zilizotolewa na kipanga njia pasiwaya.

  1. Donoa kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Teua Wi-Fi (Inapendekezwa).

    Iwapo tayari kichapishi kimeunganishwa na Ethaneti, teua Kipangishi njia.

  3. Donoa Anza Kusanidi.

    Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Donoa Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.

    Iwapo kichapishi tauari kimeunganishwa kwa Ethaneti, donoa Badilisha kwa muunganisho wa Wi-Fi., na kisha uteue Ndiyo baada ya kuangalia ujumbe.

  4. Teua Sogora ya Kusanidi Wi-Fi.

  5. Teua SSID kwa kipanga njia pasiwaya.

    Kumbuka:
    • Iwapo SSID unayotaka kuunganisha kwayo haionyeshwi kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, donoa Tafuta Tena ili kusasisha orodha. Iwapo bado haitaonyeshwa, donoa Ingiza Kikuli, na kisha uingize SSID moja kwa moja.

    • Iwapo hujui jina la mtandao (SSID) angalia iwapo maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Iwapo unatumia kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio yake chaguo-msingi, tumia SSID kwenye lebo. Iwapo huwezi kutafuta maelezo yoyote, tazama nyaraka zilizotolewa pamoja na kipanga njia pasiwaya.

  6. Donoa Ingiza Nywila, na kisha uingize nenosiri.

    Kumbuka:
    • Nenosiri linaathiriwa na herufi ndogo na kubwa.

    • Iwapo hujui nenosiri, angalia iwapo maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Kwenye lebo, nenosiri linaweza kuandikwa “Network Key”, “Wireless Password”, na kadhalika. Iwapo unatumia kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio chaguo-msingi, tumia nenosiri lililoandikwa kwenye lebo.

  7. Unapokamilishai, donoa OK.

  8. Angalia mipangilio, na kisha udonoe Anza Kusanidi.

  9. Donoa Sawa ili kukamilisha.

    Kumbuka:

    Ukishindwa kuunganisha, pakia karatasi tupu la ukubwa wa A4, na kisha uteue Chapisha Ripoti ya Ukaguzi ili kuchapisha ripoti ya muunganisho.

  10. Funga skrini ya Mipangilio ya Muunganis. Mtandao.