> Kuchapisha > Kuchapisha Picha > Kuchapisha Faili za TIFF kutoka kwenye Kifaa cha Kumbukumbu > Chaguo Mahiri za Menyu kwa Mipangilio ya TIFF

Chaguo Mahiri za Menyu kwa Mipangilio ya TIFF

Kumalizia:
  • Kumalizia

    Teua Pangiliza (Mpang'o wa Ukurasa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi zilizochanganywa kwa mpangilio na kupangwa kwenye vikundi. Teua Kikundi (Kurasa Sawa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi kwa kupata kurasa zenye nambari sawa kama kikundi.

  • Toa Karatasi

    Kawaida imeteuliwa.

Ubora:

Teua Bora kwa ubora wa juu wa uchapishaji, lakini kasi ya uchapishaji inaweza kupungua.

Agizo la Chapa:

Teua mpangilio ya uchapishaji wa kurasa anuwai wa faili TIFF.

Tarehe:

Teua umbizo la tarehe ambayo picha ilipigwa au kuhifadhiwa. Tarehe haichapishwi kwa baadhi ya miundo.

Kuhifadhi Faili

Unaweza kuhifadhi data ya uchapishaji kwenye hifadhi.

  • Mpangilio:

    Chaguo iwapo utahifadhi data ya uchapishaji pekee kwenye hifadhi au la.

  • Kabrasha (Inahitajika):

    Chagua folda ambapo utahifadhi data ya uchapishaji.

  • Jina la Faili:

    Weka jina la faili.

  • Nenosiri la Faili:

    Weka nenosiri ili kuchagua faili.

  • Jina la Mtumiaji:

    Weka jina la mtumiaji.