
|
Vipengele |
Mipangilio na Ufafanuzi |
|
|---|---|---|
|
Authentication Method |
Bainisha mbinu ya uhalalishaji kwa kichapishi ili kufikia seva ya barua. |
|
|
Off |
Weka wakati seva ya barua haihitaji uhalalishaji. |
|
|
SMTP AUTH |
Huhalalishwa kwenye seva ya SMTP (seva ya barua inayoondoka) unapotuma barua pepe. Seva ya barua inahitaji kuauni uhalalishaji wa SMTP. |
|
|
POP before SMTP |
Huhalalisha kwenye seva ya POP3 (seva ya kupokea barua) kabla ya kutuma barua pepe. Unapoteua kipengee hiki, weka seva ya POP3. |
|
|
Authenticated Account |
Ukiteua SMTP AUTH au POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza jina la akaunti ya uhalalishaji kati ya vibambo 0 na 255 kwenye ASCII (0x20–0x7E). Unapoteua SMTP AUTH, ingiza akaunti ya seva ya SMTP. Unapoteua POP before SMTP, ingiza akaunti ya seva ya POP3. |
|
|
Authenticated Password |
Iwapo utateua SMTP AUTH au POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza nenosiri lililohalalishwa kati ya vibambo 0 na 20 kwenye ASCII (0x20–0x7E). Unapoteua SMTP AUTH, ingiza akaunti iliyohalalishwa kwa seva ya SMTP. Unapoteua POP before SMTP, ingiza akaunti iliyohalalishwa kwa seva ya POP3. |
|
|
Sender's Email Address |
Ingiza anwani ya barua pepe ya mtumaji kama vile anwani ya barua pepe ya msimamizi wa mfumo. Hii inatumika unapohalalisha, kwa hivyo ingiza anwani halali ya barua pepe iliyosajiliwa kwenye seva ya barua. Ingiza kati ya vibambo 0 na 255 kwenye ASCII (0x20–0x7E) isipokuwa kwa : ( ) < > [ ] ; ¥. Kitone “.” hakiwezi kuwa kibambo cha kwanza. |
|
|
SMTP Server Address |
Ingiza vibambo kati ya 0 na 255 kwa kutumia A–Z a–z 0–9 . -. Unaweza kutumia umbizo la IPv4 au FQDN. |
|
|
SMTP Server Port Number |
Ingiza nambari kati ya 1 na 65535. |
|
|
Secure Connection |
Teua mbinu ya usimbaji fiche wa mawasiliano kwenye seva ya barua. |
|
|
None |
Iwapo utateua POP before SMTP kwenye Authentication Method, muunganisho haujasimbwa fiche. |
|
|
SSL/TLS |
Hii inapatikana wakati Authentication Method imewekwa kwa Off au SMTP AUTH. Mawasiliano yanasimbwa fiche kutoka mwanzo. |
|
|
STARTTLS |
Hii inapatikana wakati Authentication Method imewekwa kwa Off au SMTP AUTH. Mawasilano hayasimbwi fiche kutoka mwanzo, lakini kulingana na mazingira ya mtandao, iwapo mawasiliano yamesimbwa fiche au la yanabadilishwa. |
|
|
Certificate Validation |
Cheti kinahalalishwa hii inapowezeshwa. Tunapendekeza hii iwekwe kwa Enable. Ili kusanidi, unahitaji kuleta CA Certificate kwenye kichapishi. |
|
|
POP3 Server Address |
Ukiteua POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza anwani ya seva ya POP3 kati ya vibambo 0 na 255 kwa kutumia A–Z a–z 0–9 . -. Unaweza kutumia umbizo la IPv4 au FQDN. |
|
|
POP3 Server Port Number |
Ukiteua POP before SMTP kama Authentication Method, ingiza nambari ya kati ya 1 na 65535. |
|