> Kuchapisha > Kuchapisha Nyaraka > Kuchapisha kutoka kwenye Kompyuta — Windows > Kuchapisha kwa Kutumia Kipengele cha Uchapishaji Uliosawazishwa

Kuchapisha kwa Kutumia Kipengele cha Uchapishaji Uliosawazishwa

Unaweza kuboresha uonekanaji wa matini na picha kwenye machapisho.

Chapisho Lote la Rangi kinapatikana tu mipangilio ifuatayo inapoteuliwa.

  • Aina ya Karatasi: Karatasi tupu 1, Karatasi tupu 2, Karatasi ya barua, Iliyotumiwa tena, Rangi, Iliyochapishwa awali, Karatasi tupu ya Ubora wa Juu, Karatasi nene 1, Karatasi nene 2, Karatasi nene 3 au Karatasi nene 4

  • Ubora: Wastani au ubora wa juu

  • Rangi ya Kuchapisha: Rangi

  • Proghramu-tumizi: Microsoft® Office 2007 au toleo la baadaye

  • Ukubwa wa Matini: Alama 96 au kidogo

  1. Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi cha Chaguo Zaidi, bofya Chaguo za Taswira kwenye mpangilio wa Usahihishaji wa Rangi.

  2. Teua chaguo kutoka kwenye mpangilio wa Chapisho Lote la Rangi.

  3. Chaguo za Uboreshaji ili uunde mipangilio zaidi.

  4. Weka vipengee hivyo vingine kwenye Kuu, Kukamilisha au vichupo vya Chaguo Zaidi inavyohitajika, kisha ubofye SAWA.

    Kichupo cha Kuu

    Kichupo cha Kukamilisha

    Kichupo cha Chaguo Zaidi

  5. Bofya Chapisha.

    Kumbuka:
    • Baadhi ya vibambo vinaweza kubadilishwa kwa ruwaza, kama vile “+” uonekana kama “±”.

    • Ruwaza na mistari ya chini maalum ya programu-tumizi inaweza kubadilisha maudhui yaliyochapishwa kwa kutumia mipangilio hii.

    • Ubora wa chapisho unaweza kupungua kwenye picha na taswira nyingine unapotumia mipangilio ya Chapisho Lote la Rangi.

    • Kasi ya uchapishaji inapungua unapotumia mipangilio ya Chapisho Lote la Rangi.