> Utambazaji > Kutambaza Nakala Asili hadi kwenye Kabrasha ya Mtandao > Chaguo za Menyu za Kutambaza kwenye Kabrasha

Chaguo za Menyu za Kutambaza kwenye Kabrasha

Kumbuka:

Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.

Hariri Eneo:

Ingiza njia ya kabrasha na uweke kila kipengee kwenye skrini.

  • Hali ya Mawasiliano:

    Teua modi ya mawasiliano ya folda.

  • Eneo (Linahitajika):

    Ingiza njia ya folda ya kuhifadhi picha iliyochanganuliwa.

    Kuteua Vinjari hutafuta kabrasha kwenye kompyuta zilizounganishwa kwenye mtandao. Unaweza tu kutumia Vinjari wakati Hali ya Mawasiliano imewekwa kuwa SMB.

  • Jina la Mtumiaji:

    Ingiza jina la mtumiaji ili kuingia kwa folda iliyoobainishwa.

  • Nenosiri:

    Ingiza nywila inayolinagana na jina la mtumiaji.

  • Hali ya Muunganisho:

    Teua modi ya muunganisho ya folda.

  • Nambari ya Kituo:

    Ingiza nambari ya kituo ya folda.

  • Mipangilio ya Seva ya Proksi:

    Teua iwapo unataka kutumia seva ya proksi au la.

Ny'i na Ny'pe/Rangi

Chagua ikiwa utatambaza kwenye monokromu au kwa rangi.

Umbizo la Faili:

Teua umbizo ambalo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.

Unapotumia PDF, PDF/A au TIFF kama ubizo la faili, teua iwapo utahifadhi nakala zote asili kama faili moja (kurasa-nyingi) au uhifadhi kila nakala asili pekee yake (ukurasa mmoja).

  • Mgao wa Mfinyazo:

    Teua kiwango cha kufinyaza picha iliyotambazwa.

  • Mipangiliuo ya PDF:

    Unapoteua PDF kama mpangilio wa kuhifadhi umbizo, tumia mipangilio hii kulinda faili za PDF.

    Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kufungua, weka Nenosiri la Kufungua Hati. Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kuchapisha au kuhariri, weka, Nenosiri la Vibali.

Mwonekano:

Teua mwonekano wa utambazaji.

Pande 2:

Tambaza pande zote za nakala asili.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

  • Ufungaji(Asili):

    Teua mwelekeo wa kuweka pamoja wa nakala asili.

Eneo la Kutambaza:

Teua eneo la kutambaza. Ili kutambaza katika eneo nzima ya glasi ya kitambazaji, teua Upeo wa Eneo.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

Aina Asili:

Teua aina ya nakala yako asili.

Mwelekeo (Asili):

Teua mwelekeo wa nakala asili.

Na. Asili zina Mch'o:

Unaweza kuweka mchanganyiko ufuatao wa ukubwa kwenye ADF kwa wakati mmoja. A3 na A4; B4 na B5. Unapotumia michanganyiko hii, nakala asili zinatambazwa kwa ukubwa halisi wa nakala asili. Weka nakala zako asili kwa kupanga upana wa nakala asili kama ilivyoonyeshwa hapa chini.

Uzito:

Teua ulinganuzi wa taswira iliyotambazwa.

Ondoa Mand'yuma:

Teua ukolevu wa mandharinyuma. Donoa + ili kuongeza mwangaza (weupe) kwenye mandharinyuma na udonoe - ili kuikoleza (kuongeza weusi).

Iwapo utateua Otomatiki, rangi za mandharinyuma za nakala asili zimetambuliwa, na zinaondolewa au kufifishwa kiotomatiki. Haitekelezwi sahihi iwapo rangi ya mandharinyuma ni kolevu zaidi au haijatambulika.

Ondoa Kivuli:

Ondoa vivuli vya nakala asili ya ambavyo vinaonekana katika taswira iliyotambazwa.

  • Fremu:

    Ondoa vivuli katika ukingo wa nakala asili.

  • Katikati:

    Ondoa vivuli vya pambizo za kuweka pamoja vya kijitabu.

  • Ukurasa wa Nyuma:

    Weka kila eneo la upande wa nyuma unapotambaza nakala asili za pande 2.

Ondoa Mash. Panchi:

Ondoa mashimo ya panji ambayo yanaonekana kwenye taswira iliyotambazwa. Unaweza kubainisha eneo la kufuta mashimo ya panji kwa kuingiza thamani kwenye kikasha upande wa kulia.

  • Mkao wa Kufuta:

    Teua mkao ili kuondoa mashimo.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

Uta'ji Unao'a ADF:

Unaweza kuweka idadi kubwa ya nakala asili kwenye ADF katika bechi, na kuzitambaza kama kazi moja ya utambazaji.

Kuhifadhi Faili:

Unaweza kuhifadhi taswira iliyotambazwa kwenye hifadhi.

  • Mpangilio:

    Chaguo iwapo utahifadhi taswira iliyotambazwa pekee kwenye hifadhi au la.

  • Kabrasha (Inahitajika):

    Teua hifadhi ambapo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.

  • Jina la Faili:

    Weka jina la faili.

  • Nenosiri la Faili:

    Weka nenosiri ili kuchagua faili.

  • Jina la Mtumiaji:

    Weka jina la mtumiaji.

Jina la Faili:
  • Kiambishi awali cha Jina la faili:

    Ingiza kiambishi awali cha jina la taswira katika vibambo vya alfanumeriki na alama.

  • Ongeza Tarehe:

    Ongeza tarehe ya jina la faili.

  • Ongeza Muda:

    Ongeza muda kwenye jina la faili.