> Kunakili > Mbinu Zinazopatikana za Kunakili > Kufuta Vibambo Vyekundu wakati wa Kunakili

Kufuta Vibambo Vyekundu wakati wa Kunakili

Unaweza kutoa nakala na vibambo vyovyote vyekundu katika nakala asili zilizofutwa.

Kumbuka:
  • Ukiteua Rangi kama mtindo wa rangi, nakala yenyewe itakuwa katika rangi moja, lakini inahesabiwa kama nakala ya rangi.

  • Ukiteua Otomatiki kama mtindo wa rangi na kitambaza kimegundua kuwa nakala asili ni ya rangi, inahesabiwa kama nakala ya rangi hata kama nakala yenyewe ni ya rangi moja.

  • Kulingana na asili, vibambo vyekundu huenda visifutwe.

  1. Weka nakala za kwanza.

    Kuweka Nakala Asili

  2. Teua Nakili kwenye skrini ya nyumbani.

  3. Teua kichupo cha Mahiri, na kisha uwezeshe Futa rangi nyekundu.

    Kumbuka:

    Skrini ya uhakiki inaonyesha picha ya asili kabla ya vibambo vyekundu kufutwa.

  4. Donoa .