Kuchapisha kwenye Upande Mmoja kwa Kutaja Kurasa na Vyanzo Anuwai vya Karatasi

Unaweza kuchapisha kwa kutaja kurasa na vyanzo anuwai vya karatasi Kitengo hiki hutumia utaratibu wa kuchapisha kwenye karatasi tofauti ya rangi ilivyoonyeshwa kwenye jedwali kama mfano.

  1. Pakia karatasi ya kuchapisha katika printa ilivyoonyeshwa hapo chini.

    Kaseti ya 1 ya Karatasi: karatasi nyeupe (karatasi wazi), Kaseti ya 2 ya Karatasi: karatasi ya waridi, Kaseti ya 3 ya Karatasi: karatasi ya manjano, Kaseti ya 4 ya Karatasi: karatasi ya kijani

  2. Fungua faili unayotaka kuchapisha kwenye kompyuta yako.

  3. Onyesha kichupo cha Kuu kwenye skrini ya kiendesha printa, na kuteua Zima kutoka kwa Uchapishaji wa Pande 2.

  4. Teua Weka tofauti kwa kila karatasi kutoka Chanzo cha K'tasi.

  5. Kwenye skrini iliyoonyeshwa, weka Jalada la Mbele/Ukurasa wa Kwanza, Kurasa Nyingine, na Jalada la Nyuma/Ukurasa wa Mwisho.

    • Katika Jalada la Mbele/Ukurasa wa Kwanza, weka chanzo cha karatasi kwa ukurasa wa kwanza na kama unachapisha au la. Katika mfano huu, teua Kaseti ya 1 ya Karatasi na Chapisha.
    • Katika Kurasa Nyingine, weka chanzo cha karatasi ambacho kinatumika sana kwa kurasa 2 hadi 9. Kwa mfano huu, teua Kaseti ya 1 ya Karatasi au Sawa na Karatasi ya Kwanza ili kubainisha karatasi nyeupe (karatasi wazi) kwenye kurasa za 2, 5, 6, 8, na 9. Mbinu ya kubainisha karatasi ya rangi katika kurasa za 3, 4, na 7 imefafanuliwa katika hatua ya 6 na hatua zinazofuata.
    • Angalia Jalada la Nyuma/Ukurasa wa Mwisho na uweke chanzo cha karatasi kwa ukurasa wa 10 na kama unachapisha au la. Katika mfano huu, teua Kaseti ya 1 ya Karatasi au Sawa na Karatasi ya Pili, na Chapisha.
  6. Fanya mipangilio ya kina zaidi kwa karatasi ya pili na zinazofuata (kurasa 2 hadi 9). Teua Karatasi Tupu/Kifungu na kubofya Mipangilio ili kufungua skrini ya mipangilio ya kina.

  7. Ingiza nambari ya ukurasa wa kuchapishwa kwa kutaja chanzo cha karatasi katika Kurasa.

    Kurasa: 3

  8. Teua chanzo cha karatasi unachotaka kutumia katika kurasa zilizobainishwa kutoka Chanzo cha K'tasi.

    Chanzo cha K'tasi: Kaseti ya 2 ya Karatasi

  9. Chagua Chapisha Kurasa za Kifungu, na ubofye Hifadhi.

  10. Fuata hatua za 7 hadi 9 ili kuhifadhi kurasa maalum zinazofuata na mipangilio ya chanzo cha ukurasa.

    Kurasa: 4, Chanzo cha K'tasi: Kaseti ya 3 ya Karatasi

    Kurasa: 7, Chanzo cha K'tasi: Kaseti ya 4 ya Karatasi

  11. Bofya SAWA, ili kufunga skrini ya Mipangilio ya Karatasi Tupu/Kifungu, na kisha ubofye SAWA ili ufunge skrini ya Mipangilio ya Chanzo cha Karatasi.

  12. Weka vipengee hivyo vingine kwenye Kuu, Kukamilisha au vichupo vya Chaguo Zaidi inavyohitajika, kisha ubofye SAWA.

    Kichupo cha Kuu

    Kichupo cha Kukamilisha

    Kichupo cha Chaguo Zaidi

  13. Bofya Chapisha.