Kuhifadhi na Kusambaza Faksi Zilizopokewa

Muhtasari wa Vipengele

Iwapo shirika lako lina msimamizi wa kichapishi, wasiliana na msimamizi wako ili kuangalia hali ya mipangilio ya kichapishi.

Kuhifadhi Faksi zilizopokewa kwenye Kichapishi

Faksi zilizopokewa zinaweza kuhifadhiwa kwenye kichapishi, na unaweza kuvitazama kwenye skrini ya kichapishi. Unaweza kuchapisha tu faksi unazotaka kuchapisha au kufuta faksi zisizohitajika.

Kuhifadhi na/au Kusambaza Faksi Zilizopokewa katika Mafikio Kando na Kichapishi

Yafuatayo yanaweza kuwekwa kama mafikio.

  • Kompyuta (mapokezi ya PC-FAKSI)

  • Kifaa cha kumbukumbu ya nje

  • Anwani ya barua pepe

  • Kabrasha lililoshirikiwa kwenye mtandao

  • Mashine nyingine ya faksi

Kumbuka:
  • Data ya faksi inahifadhiwa kama umbizo la PDF au TIFF.

  • Hati za rangi haziwezi kusambazwa kwenye mashine nyingine ya faksi. Huchakatwa kama hati ambazo zilishindwa kusambazwa.

Kupanga Faksi Zilizopokewa na Hali kama Anwani ndogo na Nywila

Unaweza kupanga na kuhifadhi faksi zilizopokewa kwenye Kikasha pokezi chako au vikasha vya bodi ya matobo. Unaweza pia kusambaza faksi zilizopokewa katika mafikio Kando na kichapishi.

  • Anwani ya barua pepe

  • Kabrasha lililoshirikiwa kwenye mtandao

  • Mashine nyingine ya faksi

Kumbuka:
  • Data ya faksi inahifadhiwa kama umbizo la PDF au TIFF.

  • Hati za rangi haziwezi kusambazwa kwenye mashine nyingine ya faksi. Huchakatwa kama hati ambazo zilishindwa kusambazwa.

  • Unaweza kuchapisha seti ya masharti ya kuhifadhi/kusambaza kwenye kichapishi. Teua Faksi kwenye skrini ya nyumbani, na kisha uteue (Menyu) > Ripoti ya Faksi > Orodha ya Masharti ya Hifadhi/Sambaza.