Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu, Kukamilisha, na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.
Rejesha mipangilio yote katika thamani chaguomsingi za kiwanda. Mipangilio kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi pia inawekwa upya kwa chaguo-msingi yake.
Teua iwapo utarejesha data ya chapisho kwenye kichapishi.
Nenosiri hulinda nyaraka za siri unapochapisha. Iwapo utatumia kipengele hiki, data ya kuchapisha inahifadhiwa kwenye kichapishi na inaweza kuchapishwa tu baada ya nenosiri kuingizwa kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi. Bofya Settings ili kubadilisha mipangilio.
Unapochapisha nakala nyingi, hukuwezesha kuchapisha nakala moja ili kuangalia maudhui. Ili kuchapisha baada ya kutoa nakala ya pili, endesha paneli dhibiti ya kichapishi.
Bofya Mipangilio ili kuweka Jina la Mtumiaji na Jina la Kazi.
Hukuwezesha kuhifadhi kazi ya uchapishaji kwenye kumbukumbu ya kichapishi. Unaweza kuanza kuchapisha kwa kuendesha paneli ya udhibiti ya kichapishi.
Bofya Mipangilio ili kuweka Jina la Mtumiaji na Jina la Kazi.
Teua chanzo cha karatasi ambacho karatasi huingizwa. Teua Uteuzi Otomatiki ili kuteua kiotomatiki chanzo cha karatasi kilichoteuliwa kwenye mipangilio ya kichapishi. Ukiteua Weka tofauti kwa kila karatasi, unaweza kuteua iwapo utachapisha kwenye jalada la mbele na jalada la nyuma au la. Unaweza pia kuteua vyanzo anuwai vya karatasi kwa kurasa kwenye waraka wako. Ukiteua Karatasi Tupu/Kifungu, na kisha ubofye Mipangilio, unaweza kuweka mipangilio ya kina.
Teua trei towe unayotaka kutumia kwa machapisho. Trei towe inaweza kuteuliwa kiotomatiki kulingana na mipangilio mingine ya uchapishaji.
Teua jinsi ya kupanga nakala nyingi.
Huweka kwenye mpororo machapisho mbadala kwenye mwelekeo wa taswira na mwelekeo wa mandhari. Ili kutumia kipengele hiki, teua Uteuzi Otomatiki kama mpangilio wa Chanzo cha K'tasi na Uteuzi Otomatiki au Trei ya Kuangalisha Chini kama mpangilio wa Trei ya Zao. Machapihso yanawekwa kwenye mpororo kwenye trei inayoangalia upande wa chini.
Wakati ukubwa wa waraka ufuatao umechanganywa, huweka kwenye mpororo machapisho kwa kupanga ukingo mfupi wa karatasi kubwa na ukingo mrefu wa karatasi ndogo. Teua Bainisha Mwelekeo, na kisha ubofye Mipangilio ili kuweka mwelekeo wa karatasi na pambizo ya uunganishaji.
A3/A4
Leja/Herufi
B4/B5
8K/16K