Kuwa makini unaposhughulikia katriji zilizotumika za wino, kwani kunaweza kuwa na wino kando ya lango la kutoa wino.
Wino ukikumwagikiwa kwenye ngozi, safisha sehemu hiyo vizuri ukitumia sabuni na maji.
Wino ukiingia ndani ya macho yako, yamwagie maji mara moja. Maumivu au matatizo ya kuona yakiendelea baada ya kuyamwagia maji, mtembelee daktari mara moja.
Wino ukiingia mdomoni mwako, mtembelee daktari mara moja.
Usifungue katriji ya wino na kisanduku cha ukarabati; la sivyo wino unaweza kuingia ndani ya macho yako au kukumwagikia kwenye ngozi.
Usitikise katriji za wino kwa nguvu; la sivyo wino unaweza kuvuja kutoka kwenye katriji ya wino.
Weka katriji za wino na kisanduku cha ukarabati mbali na watoto.
Usiruhusu ukingo wa karatasi kuteleza kwenye ngozi yako kwa sababu ukingo wa karatasi unaweza kukukata.