Kuunda Mipangilio ya Kuzuia Faksi Taka

Unaweza kuzuia faksi taka.

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Faksi ya Kukataliwa.

  3. Weka masharti ya kuzuia faksi taka.

    Teua Faksi ya Kukataliwa, na kisha uwezeshe chaguo zifuatazo.

    • Orodha ya Nambari Zilizozuiwa: Hukataa faksi ambazo ziko kwenye Orodha ya Nambari ya Ukataaji.
    • Kijajuu cha Faksi kiko Tupu: Hukataa faksi ambazo zina maelezo tupu ya kijajuu.
    • Mp. simu hay. ktk W'ni: Hukataa faksi ambazo hazijaongezwa kwenye orodha ya mwasiliani.
  4. Donoa ili kurudi kwenye skrini ya Faksi ya Kukataliwa.

  5. Iwapo unatumia Orodha ya Nambari Zilizozuiwa, teua Hariri Orodha ya Nambari Zilizozuiwa, na kisha uhariri orodha.