Kuangalia Hali Ya Muunganisho

Tumia EPSON Status Monitor 3 kuangalia hali ya muunganisho ya kompyuta na kichapishi.

Unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuwezesha kipengele hiki. Unaweza kuipakua kutoka kwenye tovuti ya Epson.

  1. Fikia kiendeshi cha kichapishi.

    • Windows 10/Windows Server 2019/Windows Server 2016
      Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Mfumo wa Windows > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi kwenye Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uteue Mapendeleo ya uchapishaji.
    • Windows 8.1/Windows 8/Windows Server 2012 R2/Windows Server 2012
      Teua Eneo Kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uteue Mapendeleo ya uchapishaji.
    • Windows 7/Windows Server 2008 R2
      Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.
  2. Bofya kichupo cha Utunzaji.

  3. Bofya EPSON Status Monitor 3.

Viwango vya wino unaosalia vikionyeshwa, muunganisho umefaulu kuwekwa kati ya kompyuta na kichapishi.

Angalia yafuatayo ikiwa muunganisho haujawekwa.