Unaweza kuhifadhi faili kwenye kitengo cha diski kuu iliyojengwa ndani ya kichapishi ili kutazama, kuchapisha au kuzitoa wakati wowote.
Nafasi ambapo unaweza kuhifadhi faili inaitwa “folda”.
Kuhifadhi faili zinzotumika mara kwa mara hukuruhusu kuchapisha faili haraka na kwa urahisi au kuziambatisha kwneye barua pepe bila kutumia kompyuta.

Data iliyo kwenye folda inaweza kupotea au kuingiliwa katika hali zifuatazo.
Wakati imeathiriwa na umeme thabiti au kelele za kielektroniki.
Ikitumika visivyo
Wakati tatizo limetokea au kichapishi kimefanyiwa ukarabati
Wakati kichapishi kimeharibiwa na mkasa asilia
Epson haiwajibikii kupotea kwa data, kuingiliwa kwa data au matatizo mengine kutokana na sababu yoyote ile, hata ikiwa ni pamoja na yale yaliyojumuishwa kwenye orodha iliyo hapa juu na ndani ya kipindi cha udhamini. Pia fahamu kwamba hatuwajibikii kurejeshwa kwa data iliyopotea au iliyoingiliwa.