> Kutumia Hifadhi > Kutumia Faili kwenye Hifadhi > Kuhifadhi Faili iliyo kwenye Hifadhi kwenye Kabrasha la Mtandao au Huduma za Wingu(Chelezo)

Kuhifadhi Faili iliyo kwenye Hifadhi kwenye Kabrasha la Mtandao au Huduma za Wingu(Chelezo)

Tunapendekeza kuhifadhi faili zilizo kwenye hifadhi kwenye kabrasha la mtandao au huduma ya wingu kama chelezo.

Unahitaji kusanidi folda ya mtandao au Epson Connect kabla ya kuhifadhi.

Tazama yafuatayo unapounda kabrasha lililoshirikiwa kwenye mtandao.

Kuunda Kabrasha Lililoshirikiwa

Tazama tovuti ifuatayo ya kituo Epson Connect kwa maelezo.

https://www.epsonconnect.com/

http://www.epsonconnect.eu (Ulaya peke yake)

  1. Teua Hifadhi kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua folda iliyo na faili unayotaka kuhifadhi kwenye folda ya mtandao au huduma ya wingu, na kisha uteue Fungua.

  3. Teua faili moja.

  4. Teua Tuma/Hifadhi.

  5. Teua Kuhamisha kwenye Folda/FTP ya Mtandao au Kuhamisha kwenye Wingu.

  6. Bainisha ufikio.

    Kumbuka:

    Unapohifadhi kwenye folda ya mtandao, ingiza njia ya folda katika umbizo linalofuata.

    • Unapotumia SMB: \\jina la mpangishaji\jina la folda

    • Unapotumia FTP: ftp://jina la mpangishaji/jina la folda

    • Unapotumia FTPS: ftps://jina la mpangishaji/jina la folda

    • Unapotumia WebDAV (HTTPS): https://jina la mpangishaji/jina la folda

    • Unapotumia WebDAV (HTTP): http://jina la mpangishaji/jina la folda

  7. Weka mipangilio ya kuhifadhi ikiwa ni muhimu.

    Chaguo za Menyu kwa Tuma/Hifadhi

  8. Donoa .