Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Teua iwapo utatambaza kwenye rangi au katika rangi moja.
Otomatiki
Hutambua iwapo nakala asili ni ya rangi au monokromu, na hunakili kiotomatiki kwa kutumia modi ya rangi inayofaa zaidi.
Kulingana na nakala asili, nakala asili za monokromu zinaweza kutambuliwa kama za rangi, au nakala asili za rangi kama monokromu. Iwapo utambuzi otomatiki haufanyikazi sahihi, nakili kwa kuteua Rangi au Ny'i na Ny'pe kama modi ya rangi, au kuweka unyeti wa utambuzi. Unaweza kuweka unyeti kwa kuteua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani > Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao > Nakili Kiwango Hisi cha Rangi.
Rangi
Hunakili nakala asili katika rangi.
Ny'i na Ny'pe
Hunakili nakala asili katika rangi nyeusi na nyeupe (rangi moja).
Ongeza kiwango cha uzito wakati matokeo ya kunakili yamefifia. Punguza kiwango cha uzito wino unapomwagika.
Chagua chanzo cha karatasi ambacho unataka kutumia. Wakati Otomatiki imeteuliwa, ukubwa unaofaa unaingizwa kitomatiki kulingana na ukubwa halisi uliogunduliwa kiotomatiki na uwiano wa ukuzaji uliobainishwa.
Husanidi mgao wa ukuzaji wa upanuaji au upunguzaji. Donoa thamani na ubainishe ukuzaji unaotumika kuongeza au kupunguza nakala asili ndani ya masafa ya 25 hadi 400%.
Otomatiki
Hutambua eneo la kuchapisha na kukuza kiotomatiki au kupunguza nakala asili ili itoshee kwenye ukubwa wa karatasi uliyoteua. Wakati kuna pambizo nyeupe kwenye nakala asili, pambizo hizo nyeupe kutoka kwenye alama (
) ya kona ya kioo cha kitambazaji zinatambuliwa kama eneo la kutambaza, lakini pambizo katika upande mkabala zinaweza kupunwa.

Pu. ili Itoshee Kar'i
Hunakili picha zilizotambazwa kwa ukubwa mdogo kuliko thamani ya Punguza/Ongeza ili kutoshea ndani ya ukubwa wa karatasi. Iwapo thamani ya Punguza/Ongeza ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi, huenda data ikachapishwa zaidi ya kingo za karatasi.
Saizi Halisi
Hunakili kwa ukuzaji wa 100%.
A3→A4 na nyingine
Hukuza au kupunguza nakala asili kiotomatiki ili kutoshea kwenye ukubwa wa karatasi bainifu.
Teua aina ya nakala yako asili. Hunakili katika ubora wa juu ili kulingana na aina ya hati halisi.
Teua muundo wa pande 2.
1→Upande 1
Hunakili upande mmoja wa hati halisi kwenye karatasi ya upande moja.
2>Pande 2
Hunakili pande zote za hati halisi kwenye pande mbele ya karatasi moja. Teua mwelekeo wa nakala asili na eneo la kuunganisha nakala asili na karatasi.
1>Pande 2
Hunakili hati halisi zenye pande mbele kwenye pande mbili za karatasi moja. Teua mwelekeo wa nakala asili na eneo la kuunganisha karatasi.
2>Pande 1
Hunakili pande zote za hati halisi kwenye upande mmoja wa karatasi moja. Teua mwelekeo wa nakala yako asili na nafasi ya muunganisho ya nakala asili.
Teua muundo wa nakala.
Ukurasa Mmoja
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.
2-juu
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.
4-juu
Hunakili hati halisi zenye pande nne kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 4-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.
Teua Pangiliza (Mpang'o wa Ukurasa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi zilizochanganywa kwa mpangilio na kupangwa kwenye vikundi.

Teua Kikundi (Kurasa Sawa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi kwa kupata kurasa zenye nambari sawa kama kikundi.

Iwapo utateua Geuza Mpangilio kwenye Toa Karatasi, unaweza kuchapisha kwa njia mbadala kwenye mwelekeo wa taswira na mwelekeo wa mandhari. Chagua Otomatiki kama Mipangilio ya K'si unapotumia kipengele hiki.