Kusanidi Skrini ya Orodha ya Faili

Teua folda kwenye skrini ya Folder List kisha uteue Fungua ili utazame orodha ya faili zilizo kwenye folda.

Tafuta waraka kwa kuingiza jina la waraka au la mtumiaji.

Panga faili kulingana na vipengee. Unaweza kubadili mpangilio kati ya ndogo au kubwa.

Huonyesha vijipicha vya faili. Ikoni ya ufunguo inaonyeshwa iwapo nenosiri limewekwa kwa faili. Huashiria ni kipengele kipi ambapo faili ilihifadhiwa.

Hubadili onyesho la waraka kati ya vijipicha na orodha.

Weka idadi ya nakala za machapisho.

Huonyesha menyu ya Mipangilio ya Chapa.

Teua kufuta faili baada ya kuchapisha.

Teua kitendo unachotaka kutekeleza kama vile kukagua, kutoa au kufuta faili, au unaweza kubadilisha jina la faili, watumiaji na manenosiri kutoka hapa.

Anza kuchapisha faili.